Taarifa ya ISESCO imesema vitendo hivyo vinakiuka maadili, uhuru wa maoni na heshima ya mataifa na tamaduni. ISESCO imeongeza kuwa majarida hayo ya Ufaransa yamekiuka azimio nambari A/RES/65/224 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lililotolewa Aprili 11 mwaka 2011 ambalo linasisitiza umuhimu wa vyombo vya habari katika kustawisha utamaduni wa kuvumiliana na kuheshimu uhuru wa kidini na itikadi.
Azimio hilo pia limebainisha upinzani wa Umoja wa Mataifa kwa utumizi wa vyombo vya habari kuchochea utumiaji nguvu, chuki na kuvunjiwa heshima matukufu ya kidini.
ISESCO pia imekosoa vikali shirika linalodai kutetea haki za binadamu Human Rights Watch (HRW) ambalo limeitaka serikali ya Morocco kubatilisha uamuzi wake wa kupiga marufuku majarida hayo mawili. HRW limedai kupigwa marufuku majarida hayo ni ukiukaji wa haki za binadamu lakini shirika hilo limepuuza azimio lililotajwa hapo juu la Umoja wa Mataifa. 'Ni wazi kuwa HRW inaunga mkono vitendo vya chuki, ubaguzi na uvunjiwaji heshima matukufu ya Waislamu bilioni 1.5 duniani', imeseema taarifa ya ISESCO.
Vilevile ISESCO imeunga mkono serikali ya Morcco kuhusu kadhia hii na kutoa wito kwa serikali zote za Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC kusimama kidete katika kutetea Waislamu na Uislamu na hasa njama za kumvunjia heshima Mtume Mohammad SAW.
953023