Kwa mujibu wa tovuti ya OIC, kongamano hilo litafanyika wiki ya pili ya mwezi Mei mwaka 2012 katika mji wa Ashgabat nchini Turkmenistan.
Naibu Katibu Mkuu wa OIC anayeshughulikia masuala ya kibinadamu, Balozi wa Turkmenistan nchini Saudi Arabia na Mkuu kongamano hilo ndio wanaosimamia kongamano hilo. Kikao hicho kinafuatia kile cha hivi karibuni cha Katibu Mkuu wa OIC Prof. Ekmeleddin Ihsanoglu na Mkuu wa UNHCR.
Kongamano hilo litakalofanyika Mei 10-11 linatazamiwa kuhudhuriwa na wajumbe 400 kutoka kote duniani. Hilo litakuwa ni kongamano la kwanza la aina yake kujadili kadhia ya wakimbizi katika nchi za OIC.
952521