IQNA

Utawala wa Kizayuni unataka kuharibu sura ya Iran

16:26 - February 14, 2012
Habari ID: 2274035
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Ramin Mehmanparast amesema: 'Matukio yenye kutiliwa shaka ya hivi karibuni yaliyoratibiwa na wakuu wa utawala wa Kizayuni yenye lengo la kuharibu sura ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yameanza kutekelezwa.
Mehmanparast amekanusha madai ya utawala wa Kizayuni kuwa eti Iran imehusika katika mashambulizi ya balozi za utawala huo huko India na Georgia na kusema hayana msingi wowote, bali ni katika hila za Wazayuni za kuendeleza vita vyao vya kisaikolojia dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Mehmanparast amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni mhanga wa matukio ya kigaidi na kuongeza kuwa fitina zinazoibuliwa na utawala wa Kizayuni zinalenga kupotosha fikra za walimwengu kuhusu ugaidi unaotekelezwa na utawala huo dhidi ya Wapalestina na mauaji ya wanasayansi Wairani.
952976
captcha