IQNA

Utawala wa Kizayuni wapiga marufuku adhana mjini Nablos

16:28 - February 14, 2012
Habari ID: 2274190
Mahakama Kuu ya utawala haramu wa Israel imetoa hukumu ya kupiga marufuku adhana katika msikiti uliojengwa hivi karibuni katika kijiji cha Burin katika kiunga cha mji wa Nablos.
Kwa mujibu wa tovuti ya CPI, mahakama kuu hiyo imesema kwamba wasimamizi wa msikiti huo hawapasi kuruhusu adhana iadhiniwe kwenye msikiti huo kupitia vipaaza sauti na kwamba wanapasa pia kuzima taa zake.
Hukumu hiyo imetolewa wakati ambao waumini wanaoishi katika eneo hilo walikuwa wanajitayarisha kusimamisha swala ya kwanza ya jamaa kwenye msikiti huo baada ya kukamilika ujenzi wake. Utawala wa Kizayuni unadai kwamba msikiti huo ulijengwa kinyume cha sheria na bila kibali rasmi kutoka kwa watawala wa Kizayuni wa eneo hilo.
Kabla ya hapo utawala wa Kizayuni wa Israel ulishambulia msikiti mwingine wa Salman Farisi katika kijiji hicho hicho cha Burin na kuzuia kukamilishwa ujenzi wake. 952981
captcha