Sean Stone amesilumu katika ofisi ya Ayatullah Nassiri mjini Isfahan. Stone amekuwa mjini Isfahan kwa siku kadhaa sasa kwa ajili ya kufuatilia masuala ya utengenezaji filamu. Amesema ametumwa nchini Iran na shirika la Realnight kuhakiki na kuandaa utangulizi wa utengenezaji wa filamu ya Rumi ambayo inahusiana na maisha ya Maulana Jalalludin Balkhi Rumi, mshairi mashuhuri wa Iran. Amesema filamu hiyo ni ya Kiislamu kwa upande mmoja na ya Kiirani kwa upande wa pili.
Shirika ambalo limemtuma Sean Oliver nchini Iran lina makao makuu yake mjini Hollywood Marekani. Shirika hilo lina mpango wa kutengeneza filamu kuhusiana na Uislamu kwa lengo la kuondoa nukta na mitazamo hasi iliyoenea katika nchi za Magharibi kuhusiana na dini hii tukufu.
Oliver Stone baba yake Sean Oliver, ni mmoja wa wawekezaji mashuhri wa shirika hilo. Wana lengo la kuanza kutengeneza filamu hiyo nchini Iran chini ya waongozaji Wamarekani.
Siku ya Alkhamisi Sean Stone alitunukiwa loho ya shukrani kutoka kwa Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kikao cha kimataifa cha 'Hollywoodism na Sinema' kilichofanyika hivi karibuni mjini Tehran. 953491