Tovuti ya al Sharq imeripoti kuwa, wafanuzi 83 wa kike na kiume wa Kituo cha Qur'ani cha al Aflah walienziwa jana kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhisha Qur'ani.
Waziri wa zamani wa Usafirishaji wa Anga wa Somalia Sheikh Ali Muhammad Waren, mwakilishi wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhisha Qur'ani Tukufu Sheikh Muhammad Ahmad, walimu wa kituo hicho na kadhalika walihudhuria sherehe hiyo.
Sherehe hiyo ilianza kwa kiraa ya Qur'ani Tukufu iliyofuatiwa na hotuba za maulama na wanaharakati wa Qur'ani Tukufu ambao wamesisitiza juu ya kudumishwa mwenendo wa kuhifadhi Qur'ani na kukifanyia kazi kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu.
Mahafidhi wa Qur'ani pia wamehimizwa kushikamana barabara na kitabu hicho na kuwa kigezo bora kwa watu wa jamii. 953924