IQNA

Semina ya 'Qur'ani katika Ulimwengu wa Sasa'

12:25 - February 16, 2012
Habari ID: 2275033
Semina ya wiki moja yenye anwani ya 'Qur'ani katika Ulimwengu wa Sasa' itafanyika Marekani katika Chuo Kikuu cha Princeton, New Jersey.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA semina hiyo itafanyika kwa ajili ya wanachuo na wataalamu wanaokumbana na Uislamu katika kazi zao chuoni hapo.
Mada zitakazojadiliwa katika semina hiyo ni pamoja na tafsiri ya Qur'ani, athari ya tafsiri za Qur'ani katika maadili ya mtu binafsi, uhusiano wa kijamii na harakati za kisiasa. Aidha washiriki watajadili nafasi ya Qur'ani katika Sheria za Kiislamu, Qur'ani na Haki za Binadamu na pia Qur'ani na Vitabu Vitakatifu vya Mayahudi na Wakristo.
Semina hiyo itaongozwa na Dr. Mahan Mirza wa Chuo cha Zaytuna na Dr. Abdullah Saeed wa Chuo Kikuu cha Melbourne. Semina hiyo itafanyika kuanzia Julai 8-13.
954208
captcha