IQNA

Kongamano la kimataifa la kutetea Quds kufanyika Qatar

16:30 - February 18, 2012
Habari ID: 2276019
Kongamano la kimataifa la kutetea Quds Tukufu limepangwa kufanyika tarehe 25 na 26 za mwezi huu wa Februari katika mji mkuu wa Qatar, Doha.
Kwa mujibu wa tovuti ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Nchi za Kiislamu ISESCO, kongamano hilo ambalo limeandaliwa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, linafanyika kwa ushirikiano wa Qatar pamoja na Wapalestina wanaoishi mjini Doha.
Wanazuoni, wanafikra, wasomi, wataalamu na wawakilishi wa nchi za Kiislamu watakaoshiriki katika kongamano hilo watajadili jinai za utawala haramu wa Israel pamoja na hatua zake za kuharibu maeneo matakatifu ya Waislamu na Wakristo wa Palestina pamoja na kuwanyima haki zao za kimsingi.
Shirika la ISESCO ni moja ya mashirika muhimu yatakayoshiriki kwenye kongamano hilo la kimataifa. 955134
captcha