IQNA

Msahafu mkubwa zaidi waingia katika Rekodi za Dunia za Guinness

16:26 - February 18, 2012
Habari ID: 2276168
Tabu la Rekodi za Dunia Guinness limeutambua msahafu wenye urefu wa mita mbili ulio katika mji wa Kazan, Russia kuwa mkubwa zaidi duniani.
Qur'ani hiyo ina urefu wa mita mbili kwa mita 1.5 na ina kurasa 632 zilizotayarishwa kwa karatasi maalumu. Jildi la Msahafu huo limepambwa kwa malakati, jasper, fedha na dhahabu.
Qur'ani hiyo kubwa zaidi duniani imehifadhiwa katika Msikiti wa Kul Sharif (Qolsharif) ambao pia ni wa kipekee na kati ya misikiti mikubwa zaidi duniani.
Kazan ni mji mkuu wa Tatarstan, jamhuri inayojitawala ndani ya Shirikisho la Russia. Aghalabu ya wakazi wa Tatarstan ni Waislamu.
Serikali ya Tatarstan ndio iliyotoa ombi la kutengenezwa msahafu huo.
955200


captcha