IQNA

Mkutano wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu wafutwa Uswisi

11:37 - February 19, 2012
Habari ID: 2276729
Baraza Kuu la Waislamu wa Uswisi limetangaza kuwa mkutano wa kimataifa wa Umoja wa Kiislamu mwaka 2012 uliokuwa umepangwa kufanyika nchini humo, umefutwa.
Taarifa iliyotolewa Baraza Kuu la Waislamu wa Uswisi imesema kuwa mkutano huo ambao ulipangwa kufanyika tarehe 25 Februari ukihudhuriwa na wanafikra 1800 wa Kiislamu kutoka maeneo mbalimbali duniani umefutwa kutokana na upinzani wa viongozi wa serikali za kieneo.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa maafisa wa serikali wa miji miwili ya uswisi ambao awali walikuwa wameafikiana na maafisa wa Baraza Kuu la Waislamu wa Uswisi kuhusu jinsi ya kufanyika mkutano huo wametangaza kuwa hawatawapa Waislamu kumbi zilizotayarishwa kwa ajili ya kufanyika mkutano na kwa sababu hiyo wasimamizi wake wamelazimika kuufuta.
Baraza Kuu la Waislamu wa Uswisi ni moja ya taasisi kubwa zaidi za Kiislamu za nchi hiyo na linaongozwa na Nicolas Blancho. 955945


captcha