Kwa mujibu wa tovuti ya granadaschool, mashindano hayo huandaliwa kila mwaka na shule ya Kiislamu ya Granada kwa madhumuni ya kuwashawishi wanafunzi wajishughulishe zaidi na suala la kusoma na kuhifadhi kitabu hicho kitakatifu.
Mashindano hayo yatahusisha makundi manane ya wanafunzi wote wa shule za chekechea na za msingi.
Washiriki wa mashindano hayo wanaweza kushiriki katika kundi lolote la kuhifadhi sura zote zilizofundishwa katika shule hiyo katika kipindi cha mwaka mzima.
Waamuzi mashuhuri watatathmini juhudi za washiriki wa mashindano hayo na kisha kuwapa washindi zawadi kwa mujibu wa juhudi hizo. 956152