Kwa mujibu wa tovuti ya Lexpress kongamano hilo ambalo limeandaliwa na shirika lisilo la serikali la RAFRAM limewashirikisha shakhsia na wataalamu kutoka pembe mbalimbali za dunia.
Kongamano hilo ambalo limewashirikisha shakhsia wa kimataifa zaidi ya 6000 limewasilisha Uislamu kama njia bora ya kutatua changamoto na matatizo mbalimbali yanayomkabili mwanadamu wa leo. Kongamano hilo pia lilijadili maudhui mbalimbali kama vilevile 'mwanadamu; kiumbe aliye na pande tofauti, thamani za Kiislamu katika ulimwengu wa leo na maisha ya Kiislamu katika mwaka 2012.'
Licha ya kuweko mashinikizo ya baadhi ya makundi dhidi ya serikali ya Mauritius kwa lengo la kuilazimisha ifute kongamano hilo na kuwazuia baadhi ya wasomi wa Kiislamu kuingia nchini humo lakini kongamano hilo lilifanyika kama ilivyokuwa imepangwa awali.
Kongamano hilo limegharamiwa na jumuiya za Kiislamu na misikiti ya Mauritius. Kwa hakika kongamano hilo ilikuwa fursa nzuri kwa Waislamu wa Mauritius kufahamu thamani na mafundisho ya Kiislamu na hivyo kuzingatia zaidi hali ya Waislamu wa nchi hiyo iliyo na jamii tofauti. 956185