Ekmeleddin Ihsanoglu amesema kwamba shambulio hilo ni hujuma ya wazi ya Wazayuni dhidi ya ulimwengi mzima wa Kiislamu. Ameongeza pia kwamba huo ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa. Amesema utawala haramu wa Israel ndio unaohusika moja kwa moja na hujuma hiyo na amelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na jamii ya kimataifa kuchukua hatua za haraka kwa lengo la kuzuia kukaririwa vitendo kama hivyo dhidi ya Wapalestina wasio na hatia na maeneo yao matakatifu.
Jana asubuhi kundi moja la Mayahudi wenye misimamo ya kupindukia mipaka wakiandamana na polisi wa utawala haramu wa Israel lilivunjia heshima Msikiti wa al-Aqsa kwa kuingia msikitini humo na kuwakandamiza waumini wa Kiislamu waliokuwa wakiswali.
Mayahudi wengine walikusanyika katika Lango la Maghariba tayari kuushambulia msikiti huo mtukufu. Polisi waliokuwa hapo waliwazuia Wapalestina waliokusudia kuingia katika msikiti huo kwa madhumuni ya kuwasaidia ndugu zao waliokuwa wamezingirwa na Wazayuni. 956405