Hayo yamesemwa na Ahmad Zarnegar ambaye ni Mshauri wa Masuala ya Qur'ani katika Shirika la Iran la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu (ICRO). Ameongeza kuwa Darul Qur'ani hizo zitafunguliwa katika vituo vya utamaduni vya Iran vilivyo katika nchi mbalimbali duniani.
Ahmad Zarnegar amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa shughuli za Qur'ani zinapaswa kuimarishwa na kuwa sehemu maalumu ya shughuli za kiutamaduni.
Amesema ICRO ina mpango wa kuanzisha redio za Qur'ani katika nchi za kigeni na vilevile kuanzisha jarida maalumu kuhusu masuala ya Qur'ani.
Ahmad Zarnegar ameashiria safari yake nchini Tanzania hivi karibuni na kusema, 'Tanzania ni kati ya nchi kumi ambazo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeandaa Wiki ya Qur'ani kwa mnasaba wa Miladun-Nabii SAW.
Ameongeza kuwa washindi wa mashindano ya kitaifa ya Qur'ani yaliyofanyika Tanzania watashiriki katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran yatakayofanyika mwezi Juni mwaka huu.
956393