Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Waziri wa Utamaduni wa Tunisia ameyasema hayo mjini Tunis alipokutana na Balozi wa Iran nchini humo. Mabruk amesema utamaduni ni msingi imara wa kustawisha uhusiano wa kiutamaduni baina ya mataifa na serikali na kuongeza kuwa utamaduni ndio msingi wa matukio ya kiuchumi na kisiasa.
Amesema yuko tayari kuitembelea Iran ili kutia saini mikataba ya uhusiano wa Tehran na Tunis katika nyanja za kisayansi, kiutamaduni na kielimu. Aidha ametoa mwaliko kwa Iran kushiriki katika maonyesho ya kimataifa ya vitabu na utamaduni wa Kiislamu katika mkoa wa Al Qayrawan nchini humo. Maonyesho hayo yatanfayika katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Kwa upande wake, Balozi wa Iran nchini Tunisia Bw. Jabelo amesema Iran iko tayari kuandaa 'Wiki ya Utamaduni wa Tunisia' nchini Iran.
955959