IQNA

Chakula halali ni utangulizi wa amali njema

17:45 - February 20, 2012
Habari ID: 2277708
Kula chakula halali ni utangulizi wa kutenda amali njema na wasiozingatia suala hili hawawezi kutenda amali njema.
Haya ni kwa mujibu wa Esmaili, mtafiti wa Tiba ya Kiislamu ambaye amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa, 'chakula chochote ambacho kimepigwa marufuku katika Uislamu huwa na madhara ya kimwili na hata kiroho kwa mwanadamu'.
'Madhara mengi bado hayajagundulika lakini pamoja na hayo Waislamu wanaamini kuwa Qur'ani Tukufu ni Neno la Mwenyezi Mungu kwa hivyo wanafahamu kuwa chochote kinachokatazwa na dini kinadhuru afya', ameongeza.
Ameashiria mfano wa kuharamishwa nguruwe na pombe katika Uislamu na kuongeza kuwa: 'Katika hali ambayo viwili hivyo viliharamishwa karne 14 zilizopita, wanasayansi sasa wamegundua namna vinavyoweza kuwa hatari kwa figo, mapafu n.k.'. Ameashiria aya ya 51 ya Suratul Muuminun inayosema" Enyi Mitume! Kuleni vyakula vizuri na tendeni mema. Hakika Mimi ni Mjuzi wa mnayoyatenda". Amesema aya hii inaonyesha wazi kuwa kula vyakula halali ni utangulizi wa kutenda amali njema kwani mwili na roho vina uhusiano wa karibu.
Vilevile Ismaili amefafanua kuhusu mtazamo wa afya kwa mujibu wa Qur'ani Tukufu na kuashiria aya ya 31 ya Surat al A'araf katika Qur'ani inayosema"….na kuleni, na kunyweni na wala msifanye ubadhirifu. Kwa hakika Yeye hapendi wanaofanya israfu".
952047
captcha