Kwa mujibu wa gazeti la Sauti al Balad la Misri, mashindano hayo yaliyowashirikisha wasichana na wavulana 50 waliohifadhi Qur'ani Tukufu, yalifanyika katika Msikiti wa Istiqama kisiwani Pemba.
Mashindano hayo yamefanyika katika sehemu tano za hifdhi ya Qur'ani nzima na tartili, hifdhi ya juzuu 20, hifdhi ya juzuu 15, hifdhi ya juzuu 10 na hifdhi ya juzuu 3.
Kamati ya majaji wa mashindnao hayo iliongozwa na Sulaiman Ali Yusuf.
Washindi katika mashindano hayo walitunukiwa zawadi katika sherehe iliyohudhuriwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabhi, Mkuu wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur'ani Zanzibar Mussa Omar Said na Naibu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhisha Qur'ani Ali Bakri.
Wasomi hao wamesisitiza juu ya umuhimu wa kushikamana na Qur'ani Tukufu. 957089