IQNA

Kikao cha kwanza cha kamati huru ya haki za binadamu ya OIC chafanyika

16:05 - February 21, 2012
Habari ID: 2277997
Kikao cha kwanza cha Kamati Huru ya Kudumu ya Haki za Binadamu ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu CPIDH kimefanyika huko Jakarta, mji mkuu wa Indonesia.
Kwa mujibu wa tovuti ya jumuiya hiyo oic-oci, kikao hicho kilihudhuriwa na Ekmeleddin Ihsanoglu, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC pamoja na wawakilishi wa nchi za Kiislamu mjini Jakarta.
Akizungumza katika kikoa hicho Ihsanoglu amesema kuwa kufanyika kikao hicho cha kwanza ni nukta muhimu na ya kihistoria katika maisha ya Waislamu. Amesema kubuniwa kwa kamati hiyo katika jumuiya ya OIC ni nukta muhimu inayothibitisha kwamba Waislamu wameazimia kufanya marekebisho ya hali iliyopo na kuimarisha shughuli zao kuhusiana na suala la haki za binadamu.
Amesema licha ya kuwa kuna makundi ambayo yanaeneza duniani chuki dhidi ya mafundisho ya Kiislamu kwa lengo la kuonyesha kuwa yanakwenda kinyume na misingi ya haki za binadamu, lakini makundi hayohayo yanafahamu vyema kwamba huo ni uongo mtupu kwa sababu dini ya Uislamu ni dini ya amani na upendo.
Ihsanoglu amesema kuwa kamati hiyo mpya itaendelea kuwathibitishia walimwengu ukweli huo ulio wazi. 957432
captcha