Amesema suala hili ni muhimu hasa kwa kuzingatia kwamba hakuna tafauti za kimsingi baina ya makundi haya mawili ila baadhi ya hitilafu ndogo ndogo.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, katika mahojiano yake na Televisheni ya Satalaiti ya Al Misria, Sheikhul Azhar Ahmad Tayyib amesema Masuni wanapaswa kufanya mazungumzo na Mashia kwa maslahi ya Umma wa Kiislamu.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Al Azhar cha Misri ameongeza kuwa: 'Sisi hatuafiki kuenezwa madhehebu ya Kisuni katika jamii za Mashia na vilevile hatukubali kuenezwa madhehebu ya Shia miongoni mwa Masuni. Kunapaswa kudumishwa umoja na mshikamano katika jamii za Kiislamu ili zisisambaratike au kutumbukia katika mifarakano'.
Sheikh Ahmad Tayyib ameongeza kuwa: 'Kwa mtazamo wa Al Azhar hakuna tafauti baina ya Mashia na Masuni na watu wote wanaotamka 'Shahadatein' ni Waislamu; kwa hivyo Al Azhar inachukua msimamo wa kueneza ufahamu wa kati wa kifikra na kiitikadi'.
Sheikhul Azhar Ahmad Tayyib amekuwa akiongoza mikakati ya kukurubisha madhehebu ya Kiislamu kama sera muhimu inayofuatiliwa na Al Azhar. Kwa mara kadhaa amesisitiza kuwa tafauti za Mashia na Masuni ni katika masuala madogo madogo na kwamba makundi haya mawili ya Kiislamu hayana hitilafu za kimsingi za kiitikadi.
957476