IQNA

Iran yatoa 'Darsa za Qur'ani' kwa wanafunzi milioni 3

16:11 - February 21, 2012
Habari ID: 2278106
Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuimarisha Utamaduni wa Qur'ani amesema mpango wa 'Darsa za Qur'ani' utatekelezwa katika shule 25,000 katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Akizungumza Jumanne katika kikao cha wataalamu wa Wizara ya Elimu mjini Qum kuhusu Qur'ani, Sala na Ahul Bayt AS, mkuu wa taasisi hiyo Sheikh Ahmad Mowahidinejad amesema wanafunzi zaidi ya milioni tatu watashiriki katika mpango huo. Amesema mpango huo ni katika fremu ya kufikia malengo yaliyoainisha katika Hati ya Mabadiliko ya Kimsingi katika Wizara ya Elimu.
Sheikh Mowahidinejad ameongeza kuwa shughuli za Qur'ani zinalenga kuongeza maarifa ya wanafunzi wa shule za msingi na upili kuhusu mafundisho ya Qur'ani Tukufu. Ameongeza kuwa maafisa wa Qur'ani na wataalamu wa wizara wanajukumu muhimu katika suala hili.
Amesisitiza kuwa Wizara ya Elimu Iran inapaswa kutumia uwezo wake wote kueneza mafundisho ya Qur'ani, Sala na Ahul Bayt AS.
Hivi sasa kuna mipango mbalimbali ya kuimarisha harakati za Qur'ani katika shule za msingi, upili na vyuo vikuu kote Iran. Aidha serikali ya Iran imetenga bajeti maalumu kwa lengo la kuimarisha utamaduni wa Qur'ani katika ofisi na taasisi zote za serikali.
957455
captcha