IQNA

Oliver Stone aunga mkono kusilimu mwanae

20:59 - February 22, 2012
Habari ID: 2279182
Mtengeneza filamu mashuhuri wa Hollywood, Marekani Oliver Stone ameunga mkono hatua ya mwanae wa kiume, Sean Stone, kusilimu akiwa Iran.
Sean, ambaye amebadilisha jina lake na kuwa Ali, ameliambia gazeti la New York Post kuwa baba yake hana pingamizi lolote dhidi ya hatua yake ya kukumbatia imani ya Kiislamau.
"Baba yangu amesema, 'Allah yuko nawe'. Baba yangu anafahamu kuwa ninajaribu kujaza baadhi ya mapengo na kuleta amani", amesema Ali Stone.
Ameongeza kuwa ameshangazwa na namna hatua yake ya kusilimu ilivyopokelewa na baadhi huko Hollywood. Ali Stone amesema: 'Sikudhani nigekashifiwa. Ni kana kwamba ni jambo la jinai mtu kuwa Muislamu. Sikudhani chuki dhidi ya Uislamu imefika kina hiki. Wengine wanadai kuwa eti nimesilimu kwa sababu nimetendekezwa kifamilia au nimepotea na najaribu kujipata. Huu ni upuuzi mtupu'.
Ameongeza kuwa: 'Sijali hata nikikosolewa. Iwapo nitaweza kufungua mjadala kuhusu dini ili kuleta maelewano, basi jambo hilo litakuwa na thamani'.
Sean alisilimu Februari 14 nchini Iran katika ofisi ya Ayatullah Muhammad Nasseri Dowlatabadi katika mji wa Isfahan ambapo alichagua jina la Ali.
958326
captcha