IQNA

Morocco kupambana na propaganda dhidi ya Uislamu

17:49 - February 25, 2012
Habari ID: 2280449
Wizara ya Habari ya Morocco imetangaza kuwa imetayarisha mpango wa kupambana na propaganda chafu dhidi ya Uislamu kwa kushirikiana na wachapisha wa Ulaya.
Msemaji wa serikali ya Morocco Mustafa al Khulfi amesema kuwa Wizara ya Habari ya nci hiyo inataka kutekeleza mpango wa kukabiliana na propaganda chafu za kuwatisha watu kuhusu Uislamu na kuzuia maneno machafu dhidi ya Waislamu barani Ulaya kwa kushirikiana na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu.
Ameongeza kuwa wizara hiyo inashauriana na makampuni ya uchapishaji ya Ulaya katika uwanja huo kwa nia ya kuanzisha mapambano ya vyombo vya habari dhidi ya propaganda chafu zinazofanywa dhidi ya Uislamu.
Morocco haikutoa maelezo zaidi kuhusu mpango huo. 959654


captcha