Mehmanparast amesema kwamba, Iran haiingilii masuala ya ndani ya Syria. Amesema, Iran inapinga na kulaani vitendo vyovyote vile vya utumiaji mabavu na ambavyo vinakinzana na misingi ya haki za binadamu.
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran ameongeza kuwa, daima misimamo ya Tehran kuhusiana na matukio ya Syria ni kuunga mkono mageuzi ambayo ni kwa maslahi ya wananchi, na daima imekuwa ikipinga kwa nguvu zake zote uingiliaji wa kigeni katika masuala ya ndani ya nchi hiyo.
Hii ni katika hali ambayo Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Saud Al Faisal naye sasa amejiunga na Marekani katika kutaka magaidi wa Syria wapewe silaha zaidi ili kuiangusha serikali ya rais Bashar al Assad.
Wakati huo huo wananchi wa Syria wameanza leo wanashiriki katika kura ya maoni ya kuamua juu ya marekebisho iliyofanyiwa katiba ya Syria. Mamillioni ya Wasyria wanatazamiwa kushiriki katika zoezi hilo hii leo. Watu millioni 14 walio na umri wa zaidi ya miaka 18 wanatazamiwa kupiga kura katika vituo 13,835 nchini humo.
Rais Assad amesema ataitisha uchaguzi baada ya siku 90 iwapo katiba mpya itapitishwa. Kufanyika kura ya maoni ya katiba mpya ni ishara ya jinsi Rais Assad wa Sria alivyodhamiria kwa dhati kukidhi matakwa ya wananchi. Hata hivyo wapinzani ambao ni vibaraka wa Wazayuni na Wamagharibi wanafanya kila wawezalo ili kukwamisha mchakato wa mageuzi.
960309