Kwa mujibu wa vyombo vya kuaminika nara hizo na picha za chuki dhidi ya Waislamu zilichorwa kwenye kuta za msikiti huo na makundi yenye misimamo ya kupindukia mipaka na ya kibaguzi nchini Ufaransa.
Waumini waliofika msikitini hapo kuswali swala ya Alfajiri siku ya Jumatatu waliona nara hizo za chuki na uchochezi na kuziripoti kwa viongozi wa Kiislamu na maafisa husika wa usalama.
Viongozi wa Kiislamu wa msikiti uliotajwa wanasema kuwa nara hizo ziliandikwa na kundi moja lenye misimamo ya chuki na ubaguzi wa rangi ambalo katika miezi ya hivi karibuni limekuwa likijishughulisha zaidi na masuala ya kueneza uchochezi dhidi ya Uislamu.
Maafisa usalama wa eneo hilo wameahidi kufuatilia na kuwafikisha mahakamani wahusika wa kitendo hicho cha kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu.
Msikiti huo mwaka 2004 pia ulishambuliwa na makundi ya chuki dhidi ya Uislamu. 961110