Usama Hamdan mmoja wa viongozi waandamizi wa harakati ya Hamas amesema kuwa Utawala wa Kizayuni wa Israel ungali unaendeleza mipango yake ya ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina.
Ameongeza kwamba, hivi sasa utawala haramu wa Israel unaendeleza kwa kasi mipango yake ya kuuyahudisha mji mtakatifu wa Quds sambamba na mipango yake ya kinyama ya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu na Kikristo katika mji huo hususan msikiti mtakatifu wa al-Aqsa.
Aidha Usama Hamdan amelaani vikali vitendo hivyo vya utawala wa Kizayuni wa Israel na kuwataka Waislamu kusimama kidete katika kuutetea msikiti mtakatifu wa al-Aqswa kibla cha kwanza cha Waislamu.
960708