IQNA

Masomo ya tajwidi yatolewa Karbala

23:21 - February 27, 2012
Habari ID: 2281982
Masomo ya muda ya kiraa na tajwidi ya Qur'ani Tukufu yanaendelea kutolewa katika mji mtakatifu wa Karbala kwa hima ya Taasisi ya Qur'ani ya Haram ya Hadhrat Abbas (as) na Msikiti wa al Muntadhar.
Afisa wa kitengo cha habari cha Haram ya Imam Hussein (as) Alaa al Salami amesema kuwa masomo hayo ya kiraa ya Qur'ani Tukufu yalianza miezi minne iliyopita kwa lengo la kueneza utamaduni wa Qur'ani kati ya matabaka mbalimbali ya jamii ya Iraq.
Al Salami amemnukuu afisa anayeshughulikia masuala ya hifdhi ya Qur'ani katika Haram ya Hadhrat Abbas (as) akisema kuwa masomo hayo ya kiraa na tajwidi ya Qur'ani yanahusu kiraa, tajwidi na usahihishaji wa kiraa ya aya za Qur'ani.
Ametilia mkazo umuhimu wa masomo hayo na kusema lengo lake kuu ni kueneza sayansi ya Qur'ani, maarifa na utamaduni wa kitabu hicho kitakatifu katika jamii ya Iraq. 961611
captcha