Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudia imetoa taarifa ikimhujumu vikali Sheikh Hassan as-Saffar baada ya kukosoa hatua ya askari usalama wa nchi hiyo ya kushambulia na kuwafyatulia risasi waandamanaji wa nchi hiyo wanaofanya maandamano ya amani ya kupigania haki zao.
Katika taarifa yao ya kumtetea Hassan as-Saffar, watetezi wa haki za binadamu na waandishi 74 wa Saudi Arabia wamesema kuwa Sheikh as-Saffar ni mtu mwenye ikhalsi anayezingatia maslahi ya kitaifa na kwamba amekuwa na msimamo huohuo katika migogoro tofauti ambayo imekuwa ikiikumba nchi hiyo.
Wamekumbusha kwamba Sheikh as-Saffar ni mwanazuoni na mwanafikra ambaye daima amekuwa akiyasihi makundi tofauti ya kikabila na kimadhehebu ya Saudi Arabia kufanya mazungumzo ya maelewano na umoja kwa ajili ya kulinda maslahi ya nchi hiyo.
Mwishoni nwa taarifa yao, waandishi na wanaharakati hao wa haki za binadamu wa Saudia wamelaani hatua ya utawala wa nchi hiyo ya kumzushia tuhuma zisizo na msingi mwanafikra na shakhsia huyo mashuhuri. 962688