Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon, Hizbullah imeandaa kongamano lenye anuani ya , 'Quds, Mji Mkuu wa Wapalestina, Waarabu na Waislamu'.
Kwa mujibu wa televisheni ya Al Manar, kongamano hilo linafanyika Jumapili Machi 4 chini ya usimamizi wa Katibu Mkuu wa Hizbullah Sayyed Hassan Nasrallah.
Kongamano hilo limeandaliwa na Kamati ya Kuunga Mkono Mapambano (muqawama) wa Palestina.
Kati ya wanaohudhuria kongamano hilo ni Mufti Mkuu wa Lebanon, viongozi wa Wakristo, Wadruzi na makundi ya kisiasa.
Waandalizi wanasema kongamano hilo kati ya mengina linalenga kukabiliana na njama za Utawala wa Kizayuni wa Israel za Kuyahudisha Quds Tukufu. Aidha washiriki wanalenga kuvunja kimya cha kimataifa kuhusu kadhia ya Quds.
963677