IQNA

Kiako cha kukabiliana na uyahudishaji wa Quds chafanyika Jordan

17:05 - March 04, 2012
Habari ID: 2285409
Kikao cha kuchunguza njia za kukabiliana na mipango ya utawala haramu wa Israel ya kuyahudisha Quds Tukufu kimeanza leo Jumapili huko Amman mji mkuu wa Jordan kwa udhamini wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni wa Kiislamu ISESCO.
Kikao hicho ni cha tano kufanywa na Kamati ya Wataalamu wa Mambo ya Kale ya ISESCO. Kamati hiyo ina ushirikiano wa karibu na Idara Kuu ya Mambo ya Kale ya Jordan na Kamati ya Kitaifa ya Elumu, Sayansi na Utamaduni ya Palestina. Kikao hicho kitakachomalizika kesho Jumatatu, kitajadili uchokozi wa hivi karibuni wa utawala haramu wa Israel huko Masjidul Aqsa na Quds, ikiwa ni pamoja na kuyahudisha mji huo na kufuta athari zake za kale. Kamati ya kiufundi itatoa ripoti kuhusiana na hatua ambazo zimekuwa zikitekelezwa na utawala haramu wa Israel kwa madhumuni ya kuharibu na kufuta athari zote za kihistoria na Kiislamu katika mji mtukufu wa Quds. 965146
captcha