IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya wanafunzi wa vyuo vikuu kufanyika Najaf

12:49 - March 06, 2012
Habari ID: 2286271
Duru ya Nne ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani maalumu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu yatafanyika katika mji mtakatifu wa Najaf nchini Iraq Septemba mwaka huu wa 2012.
Kwa mujibu wa Ali Zojaji, Mkuu wa Masuala ya Utamaduni katika Jumuiya ya Jihadi ya Vyuo Vikuu Iran, baada ya duru za kwanza, pili na tatu kufanyika katika miji ya Iran ya Tehran, Isfahan na Mashhad kwa taratibu, mji wa Najaf wa Iraq umetangaza kuwa tayari kuandaa mashindano hayo.
Amesema mashindano ya mwaka huu yataandaliwa na Jumuiya ya Jihadi ya Vyuo Vikuu kwa ushirikiano na Baraza Kuu la Mashia la Waqfu nchini Iraq. Ameongeza kuwa moja ya sababu ya mashindano hayo ya Qur'ani kufanyika Najaf ni kutokana na kuwa Najaf umechaguliwa kuwa mji mkuu wa utamaduni katika ulimwengu wa Kiislamu mwaka 2012. Amesema tayari washiriki kutoka Lebanon, Syria na Pakistan wametangaza kushiriki katika mashindano hayo.
965926
captcha