IQNA

Njama za kufuta sheria za Kiislamu Minnesota Marekani zashindwa

10:08 - March 07, 2012
Habari ID: 2287190
Njama za mjumbe wa chama cha Republican za kuwasilisha muswada wa kupiga marufuku utumizi wa Sheria za Kiislamu katika jimbo la Minnesota Marekani zimefali baada ya upinzani mkali wa Waislamu.
'Haikuwa nia yangu ya kuwasilisha muswada wa sheria unaolenga kundi moja,' amesema Senator wa chama cha Republican Dave Thompson katika mahojiano na tovuti ya CBS Minnesota Machi 5.
Hatua hiyo inafuatia kikao na waandishi habari kilichokuwa kimeitishwa mapema na tawi la Minnesota la Baraza la Uhusiano wa Marekani na Uislamu (CAIR-MN). Mkutano huo pia uliwajumuisha viongozi wa dini mbali mbali ambapo walijadili hatari ya kuzuia uhuru wa kidini katika jimbo hilo.
"Tuko hapa leo kutuma ujumbe wa wazi kuwa kutostahimiliana na kubana uhuru wa kidini si katika thamani za Minnesota," amesema Munazza Humayun, mratibu wa masuala ya haki za kiraia katika CAIR.
Humayun amesema muswada wa sheria nambari S2281 uliandikwa kwa kutumia kigezo kilichowasilishwa na David Yerushalmi ambaye ni mtu mwenye chuki sana dhidi ya Uislamu na ambaye huko nyumba alichukua misimamo ya kutaka Uislamu upigwe kabisa marufuku Marekani. Yerushalmi ni Yahudi ambaye ana historia ndefu ya ubaguzi wa rangi, chuku dhidi ya wahamiaji wa kigeni na Uislamu.
Sheria za Kiislamu katika jimbo la Minnesota zinatumika kusimamia masuala ya kila siku ya Waislamu kama vile, sala, saumu, mirathi, ndoa na masuala ya kifedha. Sheria hizo hazitumiki kuwahukumu wasio kuwa Waislamu. Hadi sasa kuna majimbo matatu Marekani yanayotumia sheria za Kiislamu.
966818
captcha