IQNA

Baraza la Wanazuoni Iran lalaani kuvunjiwa heshima Qur'ani

10:52 - March 08, 2012
Habari ID: 2287844
Baraza la Wanazuoni Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kimefanyika mjini Tehran ambapo washiriki wote wamelaani vikali kitendo cha hivi karibuni cha wanajeshi vamizi wa Marekani cha kuteketeza moto nakala kadhaa za Qur'ani Tukufu nchini Afghanistan.
Katika kikao chake cha 11 mjini Tehran Baraza hilo limejadili masuala kadhaa ya nchini Iran, kieneo na kimataifa.
Akihutubia kikao hicho cha siku mbili kilichomalizika Jumatano , mwenyekiti wake, Ayatullah Mohammad Reza Mahdavi Kani amesema jamii ya kimataifa na hasa Waislamu kamwe hawatasahau jinai za Marekani huko Afghanistan na Iraq.
Amelaani kitendo cha wanajeshi wa Marekani kuchoma nakala za Qur'ani Tukufu huko Afghanistan na kusema ni jambo la kusikitisha kuona Wamarekani wangali wanaendelea kutusi matukufu ya Kiislamu.
Ayatullah Mahdavi Kani amezionya nchi za Kiarabu kuchukua tahadhari kutokana na njama za Wamagharibi za kuteka mwamko wa Kiislamu unaojiri katika eneo.
Katika taarifa yake ya mwisho Baraza la Wanazuoni Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu limetoa wito kwa Ummah wa Kiislamu kurejea katika utambulisho wake ili kuweza kukabiliana na njama za Wamagharibi za kuzusha mifarakano na kuzidisha mashinikizo ya kisiasa, kiuchumi na vitisho vya kijeshi dhidi ya Waislamu.
967367
captcha