Gazeti la al Bayan linalochapishwa Imarat limeandika kuwa, Kamati ya Kitaifa ya Kutetea Quds Tukufu huko Gaza ilitangaza katika kongamano lililofanyika jana kwamba shughuli za kutayarisha maandamano ya kimataifa ya kutetea Quds zilianza jana na kwamba zetaendelea kwa wiki kadhaa.
Ahmad Abu Halbiya ambaye ni afisa wa Kamati ya Quds katika Bunge la Palestina amesema kuwa Quds inakabiliwa na mashambulizi ya kila siku ya Israel na maeneo muhimu ya kihistoria ya mji huo yanalengwa na Wazayuni.
Ameongeza kuwa yanayofanyika huko Quds Tukufu ni jinai ya kivita na mauaji ya kimbari dhidi ya raia wa Palestina.
Abu Halbiya ameutaka umma wa Kiislamu na Kiarabu kushiriki kwa wingi katika maandamano ya kimataifa ya kutetea Quds Tukufu. 972170