IQNA

Mashia wa Misri wataka haki zao ziheshimiwe

11:15 - March 15, 2012
Habari ID: 2292047
Kiongozi wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Misri amesema katiba ya nchi hiyo inapaswa kuzingatia haki za Mashia.
Ahmad al Nafis amesema katika mahojiano na Televisheni ya Sadi al Balad amesisitiza kuwa hakupaswi kuna na ubaguzi wowote dhidi ya Mashia.
Ameongeza kuwa Chuo cha Kiislamu cha Al Azhar nchini Misri kinayatambua madhehebu ya Kishia ya Ja'afari.
"Sisi Mashia hatutaki kushiriki katika baraza linaloandika katiba mpya ya Misri. Kile ambacho tunakitaka ni kuheshimiwa haki zetu za kiraia na kusiwepo tafauti baina ya Mashia na Waislamu wengine kama ambavyo katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaheshimu haki za Masuni.".
Aidha amesisitiza kuwa 'Qur'ani wanayotumia Mashia ni sawa na inayotumiwa na Waislamu wengine'. Ameyasema hayo katika kujibu madai yasiyokuwa na msingi kuwa Mashia wana Qur'ani yao.
Kiongozi huyo wa Mashia nchini Misri pia ametangaza mpango wa kuanzisha chama cha kisiasa kitakachojulikana kama Al Tahrir.
971348
captcha