Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, baada ya kuwasilia Tehran msafara huo awali kabisa utaelekea katika Haram Takatifu ya Imam Khomeini-Mwenyezi Mungu amrehemu- ambapo wanaharakati hao watamsomea Fatiha mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Jumamosi asubuhi walio katika msafara huo watashiriki katika kikao na waandishi habari mjini Tehran. Baada ya hapo kutafanyika sherehe ya kuwashukuru washiriki itakayofanyika katika Mnara wa Milad mjini Tehran.
Vilevile Jumamosi jioni kutafanyika kongamano la kuwaenzi walio katika 'Msafara wa Kuelekea Baitul Muqadda'. Kongamano hilo litahutubiwa na Dkt. Ali Akbar Velayati mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ambaye pia Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Mwamko wa Kiislamu. Kongamano hilo litafanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Tundu la Majasusi (ubalozi wa zamani wa Marekani mjini Tehran).
'Msafara wa Kuelekea Baitul Muqaddas' ulianzia New Delhi India katika kaburi la mwanzilishi wa taifa la India Mahatma Gandhi. Msafara huo unajumuisha wanaharakati kutoka nchi mbalimbali za bara Asia kama vile Indonesia, Malaysia, India, Japan, Pakistan, Bangladesh, Iran n.k. Baada ya kutoka India msafara huo uliingia Pakistan na sasa unakaribia kufika Iran. Baada ya Iran msafara huo utaelekea Uturuki, Lebanon na Machi 30 msafara huo wa mabasi utaelekea katika nukta iliyo karibu zaidi na Baitul Muqaddas inayokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel.
Wanaharakati walio katika msafara huo wanasema wanataka kuanzisha mwamko nchini India na duniani kuhusu kadhia ya Palestina. 972285