IQNA

Nakala 5000 za Qur'ani zasambazwa Brazil

10:50 - March 18, 2012
Habari ID: 2293320
Nakala 5000 za Qur'ani Tukufu kwa lugha ya kireno zimesambazwa kote Brazil miongoni mwa Waislamu.
Kwa mujibu wa gazeti la A-Ittihad, Jumuiya ya Misaada ya Dubai imesambaza Misahafu hiyo kwa lengo la kuwawezesha Waislamu wa Brazil kufahami zaidi Kitabu cha Allah.
Uislamu uliingizwa Brazil na Waafrika waliofika huko kama watumwa ambao kuanzia mwaka 1550 waliongoza uasi mkubwa wa watumwa katika nchi hiyo ambayo ilikuwa ya pili kwa idadi ya watumwa duniani. Wimbi la pili la wahajiri Waislamu Brazil lilikuwa la Waarabu hasa kutoka Syria na Lebanon.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Pew Forum, idadi ya Waislamu Brazil inatabiriwa kuwa 204,000.

Wakati huo huo, Ahmed Mohammad Mesmar, afisa wa jumuiya hiyo, amesema katika taarifa kuwa, hivi karibuni pia walisambaza nakala 15,000 za Qur'ani Tukufu miongoni mwa Waislamu nchini Ethiopia.
973203
captcha