Hayo yamesemwa na Khalid Meshaal Mkuu wa Idara ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas wakati akizungumza katika kongamano la kimataifa la 'Quds, Historia na Matumaini' katika mji wa Doha nchini Qatar. Meshaal amesisitiza kuwa kunahitajika juhudi kubwa na kujitolea muhanga ili kuikomboa Quds.
'Palestina imeshuhudia kiwango kikubwa cha watu wanaojitolea mhanga katika historia yake. Wanamapambano hao walijitolea mhanga kwa lengo la kudumisha utambulisho wa Kiislamu na Kiarabu wa Quds,' amesema Meshaal.
Akisisitiza kuhusu umuhimu wa kudumisha umoja na mshikamano huko Palestina, ametoa wito kwa mataifa yote ya Kiarabu na Kiislamu kuwajibika kuhusu yanayojiri Quds kwa lengo la kuunusuru mji huo ambao ni turahti ya Waislamu wote.
979910