Akiwa mtoto Swadri alijifunza Qur'ani Tukufu na elimu nyingine za kidini na akafikia daraja ya ijtihad akiwa kijana.
Alikuwa mmoja wa walimu wakubwa wa chuo cha kidini mjini Najaf Iraq kiasi kwamba, nadharia zake katika elimu ya Usulu Fiqhi zilipewa umuhimu mkubwa na wasomi wengine wa Kiislamu. Msomi huyu aliyekuwa na uelewa na uwezo wa hali ya juu wa kielimu na aliuarifisha Uislamu kwa njia sahihi. K
wa kipindi kifupi Ayatullah Swadri aligeuka na kuwa kiongozi wa kifikra na kisiasa wa wananchi wa Iraq. Baada ya muda fulani utawala wa nchi hiyo ambao ulihisi hatari kutokana na harakati za Ayatullah Sadri ulimtia mbaroni na kisha kumuua shahidi mwanazuoni huyo mashuhuri pamoja na dada yake licha ya kuwepo malalamiko makubwa ya maulama na wananchi Waislamu wa Iraq. Miongoni mwa athari za msomi huyo ni pamoja na kitabu kiitwacho "Hamasa ya Nuru", "Falsafa Yetu", "Mwanadamu wa Leo na Matatizo ya Kijamii" na "Uchumi Yetu",
979771