Matukio mbalimbali ya eneo la Mashariki ya Kati ni kielelezo cha kushikamana Harakati ya Muqawama ya Hizbullah na stratijia za kuilinda Lebanon dhidi ya Utawala wa Kizayuni, amesema Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Beirut.
Katika hotuba yake katika Msikiti wa As Sayyidah Zainab SA mjini Beirut, Sheikh Ali Da'moush amesisitiza kuwa Hizbullah haitalegeza msimamo hata kidogo katika kukabiliana na sera za vitisho na kujitanua za utawala haramu wa Israel.
Amesisitiza kuwa mapambano ya Hizbullah ndio kizingiti kikubwa zaidi katika njama za Marekani na Utawala haramu wa Israel.
"Kama si mapambano ya Hizbullah, leo tungekuwa tunashuhudia vikosi vya utawala haramu wa Israel katika miji na vijiji vya Lebanon."
Sheikh Da'moush pia ameashiria kushindwa utawala wa Kizayuni wa Israel na waitifaki katika kadhia ya Syria. Amesema kufeli njama hizo dhidi ya Syria ni jambo ambalo 'limeimarisha azma na irada yetu ya kuendelea na muqawama (mapambano).
979936