IQNA

Wazayuni wavunjia heshima Quds na Msikiti wa Al Aqsa

17:35 - April 10, 2012
Habari ID: 2301576
Makumi ya walowezi wa Kizayuni wenye misimamo mikali wameingia katika eneo la kale la mji wa Quds ambapo wametekeleza vitendo vya kichochezi dhidi ya Wapalestina katika mji huo unaokaliwa kwa mabavu.
Walinzi wa Msikiti wa Al Aqsa wamethibitisha kuwa makumi ya walowezi wa Kizayuni wenye misimamo mikali waliingia katika Msikiti wa Al Aqsa mapema Jumapili na kuuvunjia heshima msikiti huo.
Imearifiwa kuwa walihujumu Msikiti wa Al Aqsa kupitia mlango wa Maghareba unaoelekea katika Ukuta wa al Buraq.
Viongozi wenye kufurutu mipaka wa Kizayuni wameachochea Wazayuni na kuwahimiza kujitokeza kwa wingi katika kile kinachotajwa kuwa 'Kupanda Juu ya Mlima wa Hekalu' katika siku ya Passover. Hii ni kaulimbiu ambayo hutumiwa na Wazayuni hao wakikusudia kuuhujumu Msikiti wa Al Aqsa na kuudhibiti kikamilifu.
Hivi karibuni Mufti wa Quds na ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina alisisitiza juu ya udharura wa kulindwa msikiti wa al-Aqsa mkabala na njama hatari za utawala wa Kizayuni wa Israel. Aliesema njama hizo ni pamoja na kuzusha mtetemeko bandia wa ardhi kwa lengo la kuuharibu Msikiti wa Al Aqsa.
Sheikh Muhammad Hussein, Khatibu wa Masjidul Aqsa aliwataka Waislamu kote ulimwenguni kuuhami msikiti huo mtakatifu na kibla cha kwanza cha Waislamu unaoandamwa na njama za maadui Wazayuni.
982400
captcha