IQNA

IDB kuanzisha benki ya Kiislamu Sudan

17:31 - April 10, 2012
Habari ID: 2301610
Benki ya Maendeleo ya Kiislamu (IDB) imetia saini mkataba kuhusu kuanzishwa benki mpya ya Kiislamu katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mkataba huo umetiwa saini kati ya IDB na Shirika la Dallah al Barak la Sudan. Kwa mujibu wa mkataba huo benki ya Kiislamu itafunguliwa Khartoum kwa uwekezaji wa awali wa dola bilioni moja.
Mkuu wa IDB Ahmad bin Muhammad Ali amesema benki hiyo mpya imeanzishwa kwa lengo kuwezesha uanzishwaji soko la mtaji miongoni mwa benki za Kiislamu na kuwasilisha ubunifu katika usimamizi wa fedha na kuanzisha soko la hisa la Kiislamu.
Aidha benki hiyo inatarajiwa kusaidia katika kuimarisha viwango vya huduma zinazotolewa kwa mujibu wa sheria za Kiislamu.
Katika miaka ya hivi karibuni mfumo wa benki za Kiislamu umeshuhudia ustawi wa kasi kote duniani.

981945
captcha