Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, wananchi wa Ethiopia wamefurahishwa na filamu za Iran ambazo zimetengenezwa Iran katika miaka ya hivi karibuni. Filamu hizo zilizofanyiwa dubbing kwa lugha ya Kiamhari na zenye maudhui za Qur'ani na kidini ni pamoja na 'Ibrahim Khalilullah', 'Issa (Yesu) Ruhullah', Nabii Yakub, 'Ufalme wa Suleiman', 'As'habul Kahf', 'Nabii Yusuf' na ' Mtakatifu Maryam '
Kiamhari ni lugha ya Kisemiti ambayo ni lugha rasmi nchini Ethiopia.
Filamu zingine za Kiirani zilizotarjumiwa kwa lugha ya Kiamhari ni pamoja na 'Watoto wa Mbinginu' iliyotayarishwa na mtengeneza filamu mashuhuri Muirani Majid Majidi na documentary yenye anwani ya 'Nyuso Saba za Iran' iliyotayarishwa na Farzin Rezaee kuhusu historia ya miaka 7000 ya Iran. Zaidi ya asilimia 40 ya wakazi wa Ethiopia ni Waislamu.
981622