Wabunge hao wamesema wanaipa himaya timu ya mazungumzo ya Iran ambayo itashikiri katika mazungumzo hayo kwa lengo la kutetea haki za nyuklia za taifa la Iran.
Kundi la 5+1 lijumuisha pamoja wanachama watano wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Ujerumani.
Makubaliano juu ya sehemu ya kufanyika duru mpya ya kikao cha mazungumzo baina ya Iran na kundi la 5+1, ambayo mara hii imepangwa kufanyika mjini Istanbul Uturuki, yamewavutia wachambuzi wengi wa masuala ya kisiasa.
Baadhi ya weledi wa mambo wanaamini kuwa lengo la Wamagharibi kuhusiana na mazungumzo hayo, ni kutaka kubainisha mitazamo yao tu isiyo ya kimantiki na kutafuta visingizio kwa ajili ya kuzusha makelele ya kipropaganda dhidi ya Iran.
Hii ni katika hali ambayo mazungumzo huwa na faida pale yanapofanyika katika misingi ya kimantiki na kuziwezesha pande mbili kubadilishana mawazo chini ya stratejia ya ushirikiano wa kuzinufaisha kiuadilifu pande husika.
983734