Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, semina hiyo imeandaliwa na Harakati ya Umoja wa Waislamu India katika Ukumbi wa Gandhi. Lengo la semina hiyo limetajwa kuwa ni kuimarisha umoja wa Waislamu na kuufanya ulimwengu ufahamu suala la mwamko wa Kiislamu.
Semina hiyo itahudhuriwa na wanazuoni wa Kishia na Kisuni pamoja na wasomi na matabaka mbalimbali ya Waislamu.
Semina hiyo itahudhuriwa na Hujjatul Islam Sadeq, mwanazuoni mwandamizi wa Kishia nchini India ambaye atazungumza kuhusu mwamko wa Kiislamu na hali ya kiuchumi ya Waislamu.
Wengine watakaozungumza katika kikao hicho ni Salman Nadwi, Javad Naqawi, Zaki Baqeri, Fadh-ul-Rahman Nadwi, Arshad Hussein, Seyyed Shoukat Abedi, Aziz Heydar na Azem Hussein.
Watafafanua kuhusu umoja katika Uislamu, kudumisha na kustawisha turathi ya Kiislamu, majukumu ya Waislamu nchini India, maadili ya Kiislamu, athari mbaya za tamaduni za kigeni katika jamii za Waislamu na nafasi ya Waislamu na haki za Waislamu nchini India.
982794