IQNA

Uingereza inachochea chuki dhidi ya Uislamu

17:53 - April 16, 2012
Habari ID: 2305975
Ripoti ya hivi karibuni ya kundi moja linalopinga ubaguzi imefichua kuwa Uingereza ina nafasi muhimu katika kuenea makundi yenye chuki dhidi ya Uislamu ambayo yalihusika na mauaji ya hivi karibuni nchini Norway.
Ripoti mpya iliyotolewa na kundi la kupinga ubaguzi lijulikanalo kama 'Hope Note Hate' inaonyesha kuwa Uingereza ni moja ya nchi za Ulaya ambazo zimechangia kwa kiasi kikubwa kueneza makundi yenye misimamo mikali yaliyo na chuki dhidi ya Uislamu. Imearifiwa kuwa makundi 22 ya kupinga Uislamu yanaendesha shughuli zao nchini Uingereza.
Ripoti hiyo ilitolewa siku moja kabla ya kuanza kusikilizwa kesi ya gaidi wa Norway Anders Behring Breivik ambaye mwaka jana aliwaua kwa umati watu 77 nchini humo.
"Macho yote wiki hii yataangazia kitendo cha Breivik Julai iliyopita, lakini tunawapuuza waliomtia motisha na hili ni kosa,' amesema Nick Lowels, mkurugenzi wa Hope Not Hate.
Julai mwaka jana Breivik aliua watu 77 katika hujuma ya bomu na ufyatuaji risasi katika mji mkuu wa Norway, Oslo na kisiwa cha karibu na hapo. Katika kujitetea, gaidi huyo Mkristo amesema alitekeleza mauaji hayo kwa lengo la eti kuilinda Norway isitekwe na Waislamu.
Saa moja kabla ya ukatili wake, Breivik aliwatumia baruapepe viongozi wenye misimamo mikali wa mirengo ya kulia nchini Uingereza na kusema atatekeleza mauaji kwa lengo la kulinda bara Ulaya lisitekwe na Uislamu.
986785
captcha