IQNA

Al Azhar yalaani dharau ya televisheni ya Mawahabi dhidi ya Shia

21:21 - April 17, 2012
Habari ID: 2307101
Wahadhari wa Chuo Kikuu cha al Azhar nchini Misri wamelaani dharau iliyofanywa na televisheni ya al Majd ya Mawahabi wa Saudi Arabia dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia na kutangaza kuwa harakati kama hizo ni njama za kuzusha fitina baina ya Waislamu.
Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha al Azhar wamesema dharau ya televisheni hiyo dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia ni kielelezo cha njama za kutaka kuzusha moto wa fitina na hitilafu kati ya Waislamu.
Taarifa ya wahadhiri hao imesema ilikuwa vyema kwa televisheni ya al Majd kuzungumzia mtazamo wa Uislamu kuhusu vazi la hijabu na si kuwasha moto wa fitina kwa kuzungumzia kile ilichodai ni mlinganisho wa vazi la hijabu baina ya Shia na Suni.
Mhadhiri Muhammad al Dasuqi wa al Azhar amesema kanali za televisheni zinapaswa kuwakusanya Waislamu katika kalima na neno moja na si kuzusha hitilafu baina yao. Amesisitiza kuwa madhehebu zote za Kiislamu zina mambo mengi yanayofanana na kuzikutanisha pamoja na kwamba viongozi wa madhehebu hizo walionesha kivitendo ushirikiano wa kielimu na kidugu baina yao.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa kanali ya televisheni ya al Majd ya Mawahabi wa Saudi Arabia imekuwa ikiendesha hujuma kali dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia kwa kadiri kwamba mtangaza wake Abdullah Daud alidai siku chache zilizopita kwamba vazi la hijabu la wanawake wa Kishia ni kwa ajili ya kuficha itikadi potofu za wafuasi wa madhehebu hiyo! 987575


captcha