Kwa mujibu wa gazeti la Al Ittihad, maonyesho hayo yalianza Aprili 28 katika hafla iliyohudhuriwa na Sheikh Sultan bin Ahmad al Qasemi, Mwenyekiti wa Shirika la Habari la Sharjah na maafisa wengine.
Maonyesho hayo yameandaliwa na Jumuiya ya Kiislamu ya Sharjah na pembizoni mwake kutakuwa na Kozi ya Nne ya Utafiti Kuhusu Nyaraka za Kale za Kiislamu.
Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo Majid Bushalibi amesema maonyesho hayo yamepangwa kwa mujibu wa malengo ya jumuiya ya Kiislamu ambayo ni kustawisha thamani za Kiislamu katika jamii.
Jumuiya hiyo imesema itachapisha majarida kuhusu kuhuisha turathi za Kiislamu na kufanya utafiti kuhusu nyaraka za kale, lengo likiwa ni kuhifadhi turathi za kidini na kiutamaduni za nchi za Kiarabu.
994924