Naibu Mwenyekiti wa FIFA amesema mashindano ya Olimpiki ya London ni fursa ya wanawake wa Kiislamu kuonyesha uwezo wao kwa walimwengu.
Naibu mpya wa Mkuu wa FIFA Ali al Hassan bin Ali amesema kuwa vazi la wanawake wa Kiislamu haliwezi kuwa kizuizi cha kushiriki katika mashindano ya Olimpiki.
Akijibu swali kwamba ni hatua gazi zilizochukuliwa kuzuia marufuku ya vazi la hijabu la wanawake wa Kiislamu katika michezo, al Hassan bin Ali amesema wanamitindo na wataalamu wa FIFA wamebuni vazi la wanawake wa Kiisalmu ambalo litatumiwa katika michezo mbalimbali baada ya kupasishwa.
Amesema mchezo wa mpira wa miguu ambao unapendwa kote duniani unapaswa kuwashirikisha watu wote.
Ni vyema kukumbusha kuwa mwaka 2007 FIFA ilipiga marufuku vazi la staha la mwanamke wa Kiislamu hijabu kwa kisingizio cha masuala ya usalama. Mwezi uliopita shirikishi hilo la mpira wa miguu duniani liliruhusu utumiaji wa vazi hilo katika michezo. 996911