Kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu, Waislamu wanatakiwa kujiepusha ni hitilafu na kuwaheshimu wengine, amesema Naibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu.
Akizungumza Tehran katika kongamano la kwanza la kimataifa la 'Dini na Mwamko wa Zama Hizi', Dkt. Mohammad Hussein Tabarraiyan ameongeza kuwa Uislamu unatetea, uadilifu, uhuru, usalama na kuheshimu thamani za wengine.
Amewasilisha makala yenye anuani ya 'Usalama wa Kidini na Kibinadamu' katika kongamano hilo.
Tabarraiyan amesema katika Uislamu, wanadamu wote ni sawa na kitu ambacho kinawafanya watu wawe bora zaidi ya wengine ni Taqwa (Kumcha Allah SWT) .
Naibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu ameongeza kuwa Mtume SAW alisisitiza juu ya udharura wa watu kuishi kwa pamoja kwa udugu na upendo.
998353