Maandamano hayo yamefanyika katika mji mdogo wa Carros karibu na mji wa Nice kusini mashariki mwa Ufaransa.
Waandamanaji hao walitangaza kufungamana kwao na Waislamu kote Ufaransa na kulaani vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu.
Huku wakiwa wamebeba mabango yasemayo, 'Kitendo hiki kisirudiwe tena', waandamanaji walitoa wito kwa maafisa wa usalama kuwatia mbaroni waliotekeleza hujuma hiyo.
Aprili 30 watu wasiojulikana walihujumu makaburi ya Waislamu huko Carros ambapo walichora nembo za kinazi za swastika na kuandika nara kama vile 'Ushindi kwa Le Pen' (kiongozi wa Chama cha Kitaifa Ufaransa kinachopinga Uislamu) na 'Waislamu Wafukuzwe'.
Baraza Kuu la Waislamu Ufaransa limesema vitendo hivyo vinatokana na mitazamo ya kibaguzi na chuki dhidi ya Uislamu.
1000189